Haruna Juma, Mpanda – Katavi.

Waziri Mkuu Mstafu, Mizengo Pinda amesema uwepo wa Wiki ya Mwanakatavi kwa kila mwaka itasaidia kuungataza Mkoa wa Katavi na fursa zilizizopo hali ambayo itachochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na mtu mmoja mmoja.

Pinda ambaye alikuwa ni mgeni  rasmi katika kilele cha Wiki ya Mwanakatavi kilichofanyika katika viwanja vya CCM Azimio mjini Mpanda, amesema kupitia tamasha hilo, Wajasiriamali na Wananchi wamepata fursa ya kujionea bidhaa zinazotengenezwa Mkoa wa Katavi pamoja na elimu ambayo ilitolewa kwenye mabanda mbalimbali.

Amesema, ”mmeitendea haki wiki hii, unapokuja kuna chakujifunza naamini wengi mtatoka na mawazo mapya pamoja na Ujuzi mbalimbali kwahiyo maonesho haya kwa upande mwingine ni chuo cha mafunzo ya aina mbalimbali ambapo mtu ukipita hutakosa kutoka na wazo fulani.”

Waziri Mkuu Mstafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.

Aidha, ameabainisha kuwa ukuaji wa Uchumi wa mkoa wa Katavi umechagizwa na uimarishaji wa Miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha lami inayoingia na kutoka Mkoa wa Katavi na kuishukuru serikali kwa kuendelea na mkakati wa Kuufungua mkoa wa Katavi kupitia miundombinu hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika Sekta za Afya, Elimu, Barabara, Umeme, Maji na Sekta nyingine.

Amesema, katika Wiki ya Mwanakatavi zaidi ya wananchi 20,000 wamejitokeza katika Mabanda Mbalimbali kwaajili ya kujiapatia elimu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujasiliamali, Biashara, Kilimo na uwekezaji kwa lengo la kuhakikisha wanakuwa na uelewa juu ya sekta hizo.

Maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi yalianza rasmi Oktoba 25, 2023 na kuhitimishwa Oktoba 31, 2023 yakipambwa na kaulimbiu inayosema “Talii, Wekeza imarisha Uchumi kwa Maendeleo Endelevu.”

Hii hapa kauli ya Bukayo Saka kwa Mikel Arteta
Robertinho kutumia mbinu za AFL jumapili