Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, inatarajia kuanza udhibiti wa Biashara holela ya mafuta, ili kulinda ubora wa mafuta, usalama wa Wananchi na majanga ya milipuko yanayoweza kutokea wakati biashara hizo zikifanyika.

Hayo yamesema na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina wakati wa uelimishaji Wananchu na Wafanyabiashara Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na kuhudhuriwa na Wenyeviti wa Serikali za vijiji, Kata na Halmashauri.

Hayo yamesema na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina.

Amesema, Wilaya ya Mbogwe inaongoza kwa ufanyaji wa Biashara holela ya mafuta ikiwemo ile iliyo maarufu kwa jina la kupiga nyoka kitu ambacho ni kosa kisheria na hatari kwa usalama wa Wananchi..

Aidha, Mhina aliwaomba wananchi kuchagamkia fursa ya kuuza mafuta kwa kuomba leseni kwani kwa kwa kanda ya ziwa EWURA imetoa leseni 575 na kati ya leseni hizo 26 wamiliki wamepewa barua za kujieleza ndani ya siku saba baada ya kubainika hawatoi huduma.

GGML yangara usiku wa Madini, yatwaa Tuzo mbili
Watendaji saba MSD wameondolewa kazini - Ummy