Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Mkoani Tanga unashirikisha wakandarasi wazawa kutoka Mkoani Kagera.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mkoani Kagera, Neema Kichiki Lugangira aliyetaka kujua ni wakandarasi wangapi kutoka Mkoani Kagera wamepata kazi katika mnyororo wa ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga.

Amesema, Wakandarasi wakuu wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga wanaendelea kushirikiana na wakandarasi wadogo, wajenzi na na wanna huduma mbalimbali katika mikoa yote inayopitiwa na Mradi.

Kapinga ameongeza kuwa jumla ya wakandarasi na watoa huduma 42 wamepata kazi mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa ujenzi wa Mradi huu ikiwemo uuzaji wa vifaa vya ujenzi, huduma za usambazaji wa mafuta, huduma za umeme na hoteli.

Robertinho atimuliwa Simba SC
Robertinho akalia kuti kavu Simba SC