Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda kwenda Chongoleni mkoani Tanga unaanza mwezi huu (Aprili 2021) na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Ameyasema hayo leo Aprili 12, 2021 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kiteto, Edward Ole Lkaita lililojoji iwapo Wizara itakuwa tayari kuongozana naye kutembelea vijiji ambavyo mradi unapita ili kuendelea kuwaandaa Wananchi kwa fursa za mradi.

Mradi huo utatoa ajira elfu kumi kwa Watanzania katika hatua za awali hadi ajira elfu 15 katika shughuli za ujenzi, za kawaida na nyinginezo, ambapo mradi huo pia utapita katika mikoa 8 wilaya 28 vijiji 127 na vitongoji 502.

Kalemani amewaomba wananchi wajitokeze kuchukua fursa kwa kuwa ziko rasmi kwa ajili ya Watanzania, huku akibainisha kwamba Wizara itaanza ziara katika Mikoa yote ambayo mradi unapita kuendelea kutoa elimu kwa Watanzania kuchukua fursa zilizopo kupitia mradi huo.

Aprili 11, Rais Samia Suluhu Hassan alishuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani mkoani Tanga.

Kiemba aitetea Young Africans
Asante Namungo FC kwa kushiriki! Karibuni siku nyingine