Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba SC, uongozi wa Young Africans umesema kuwa sasa ni zamu ya Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya Misri kuhakikisha kuwa wanapokea kichapo kutoka kwao katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika pindi watakapokutana.

Young Africans watakutana na Al Ahly katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi D ambalo linawajumuisha vigogo hao wawili pamoja na CR Belouzdad kutoka Algeria na Madeama kutoka Ghana.

Ofisa Ally Kamwe alisema: “Baada ya kuwafunga Simba SC sasa tunataka kwenda kuionyesha dunia ni namna gani Young Africans tutamfunga Al Ahly ambao walishindwa kufungana na Simba SC katika michezo waliyokutana nao.

Young Africans msimu huu tumedhamiria na tunataka kuhakikisha kuwa tunafika mbali katika michuano hii ya kimataifa ambayo watu wanatuona kama hatuwezi kufanya kitu.

“Tuna malengo makubwa ambayo tutawaonyesha watu baada ya kufanikiwa, kwa sasa hatutaki kuongea sana kwa kuwa watu hawawezi kutuelewa lakini Young Africans hii niwahakikishie mashabiki wetu kuwa watafurahi sana,” amesema Kamwe.

Kocha Kagera Sugar akataa kuvunja kambi
TARURA waifungua Kagera, mapato kuongezeka