Takribani watu 1,015,115 wameweza kupimwa VVU na kupokea majibu kupitia upimaji wa ngazi ya kituo na jamii kwa Mkoa wa Mara, katika kipindi cha kati ya mwaka 2018 hadi 2022.

Idadi hiyo, imetokana na hamasa kubwa ya upimaji kwa hiyari inayotolewa na Shirika la AMREF Tanzania kupitia mradi wake wa AFYA KAMILIFU, unaofadhiliwa na PEPFAR ambapo kupitia mradi huo zaidi ya watu 2576 wamepatiwa Dawa Kinga za VVU.

Mkurugenzi Mkazi Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu.

Idadi hiyo ni ile ya kipindi cha kati ya mwaka 2021 hadi mwaka 2022 ambapo jumla ya vitepe vya ‘JIPIME’ 54500 vimesambazwa, kwa wanajamii walio katika maeneo magumu kufikiwa na huduma za upimaji kama migodini na kwenye makambi ya wavuvi mkoani Mara.

Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuunga mkono malengo ya kimataifa juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yanayohusisha kufikia kiwango cha asilimia 95 kwenye upimaji wa VVU.

Vitepe vya kupimia UKIMWI.

Amebainisha kuwa, asilimia 95 nyingine ni za kwenye uanzishwaji wa tiba na dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI, ndani ya siku saba baada ya kugundulika na asilimia 95 kwenye uhamasishaji na ushauri nasaha kwa watu wa rika zote ifikapo mwaka 2030.

Tangu mwaka 2010, AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa kituo cha udhibiti na uzuiaji wa magonjwa cha nchini Marekani – CDC pamoja na PEPFAR, wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya mapambano dhidi ya VVU katika Mkoa wa Mara, ikiwemo utoaji wa huduma za tohara kinga kwa Wanaume na huduma za vipimo vya marudio kwa wajawazito, ili kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama.

Simba SC yakiri mambo magumu Ligi Kuu
Ahmed Ally: Nipo tayari kutimuliwa Simba SC