Endapo Mataifa yanaweza kuwa na utashi wa kisiasa na msaada muhimu wa kifedha, ili kuyashinda kabisa maradhi, basi Virusi vya na Ukimwi vinaweza kumalizika kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima ameyasema hayo na kuongeza kuwa ugonjwa huo hatari umeua watu milioni 40.4 tangu kuanza kwa janga hilo mwaka 1981 na ripoti zinaonyesha kuwa njia inayomaliza Ukimwi sio siri, lakini ni chaguo muhimu kuumaliza.

Amesema, “ripoti zinaonesha kuwa majibu ya HIV yanaweza kufanikiwa wakati yanatia nanga katika uongozi imara wa kisiasa, na endapo Mataifa yanaweza kuwa na utashi wa kisiasa na msaada muhimu wa kifedha Ukimwi utakuwa ni historia.”

Ripoti hiyo iliyotolewa na Program ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ukimwi – UNAIDS, inaonesha kuwa mwaka 2022 watu milioni 39 duniani kote walikuwa wanaishi na virusi vya ukimwi huku milioni 1.3 wakiambukizwa na watu 630,000 walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Rada za Saudi Arabia zang'ang'ana na Mahrez
Twaha Kiduku atamba kumchakaza Godi Apei