Serikali Nchini, imezitaka Jumuiya za Kimataifa zisaidie kukuza uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ili kupanua wigo wa ushiriki wa wananchi wake.

Hayo yamesema mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha tamko la Serikali kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa Jukwaa la Sauti za Nchi zinazoendelea uliofanyika kwa njia ya mtandao chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa ameliomba jukwaa hilo liangalie namna linavyoweza kushirikisha uchumi wa dunia na kuufungamanisha na uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

“Tumeliomba jukwaa hili lione namna ya kushirikisha nchi zinazoendelea kuboresha uchumi wetu ndani ya nchi kwa kukuza biashara na milango ya uwekezaji na namna nyingine zinazoweza kusaidia kuinua uchumi wetu,” amesema.

Jukwaa hilo linaziwezesha nchi zinazoendelea kujadili changamoto zinazowakabili na kupaza sauti zao ili ziweze kuwasilishwa kwenye mkutano wa kundi la nchi 20 zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi (G20) utakaofanyika Novemba 20, mwaka huu.

Mwalimu Nyerere aenziwe kwa vitendo - RC Homera
Kituo cha kupoza Umeme Chalinze kuwashwa Desemba