Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC, Augustin Matata Ponyo ametangaza kutowania tena urais na kusema badala yake atamuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na Muungano wa upinzani.

Hatua ya Ponyo inakuja kufuatia mapendekezo ya wagombea wanne wa upinzani waliokutana Afrika Kusini wiki iliyopita ambapo pia ameweka banana nia yake ya kumuunga mkono Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mfanyabiashara Moise Katumbi.

Wawakilishi hao wa vyama vya upinzani, walikutana jiji Pretoria nchini Afrika ya Kusini wiki iliyopita, kujadili njia za kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Desemba 20, 2023 utafanyika kwa njia huru na ya haki.

Aidha, wanasiasa hao pia walikuwa na majadiliano ya kumpata mgombea mmoja watakayempa ushirikiano ili aweze kuchuana na Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili madarakani.

Djuma Shaaban afunguka kilichomtoa Young Africvans
Makala: Vyombo vya Habari suluhisho ukatili wa Mtandaoni