Johansen Buberwa, Muleba – Kagera.

Moto Mkali umeunguza vifaa vyote vya Wanafunzi wa Chuo cha Kiislamu cha Umaru Ibn Khatwabi kilichopo kata na Wilayani ya Muleba Mkoani Kagera, wakati Wanafunzi hao wakiwa msikitini Alfajiri ya Novemba 19, 2023.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Abel Nyamahanga amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo cha moto huo kimetonaka na hitilafu ya umeme katika Bweni la hilo la Wanafunzi wa chuo hicho na hakuna yeyote aliyedhurika.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Abel Nyamahanga.

Amesema, “mpaka sasa Serikali kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Dkt Oscar Ishengoma Kikoyo tumetoa Magodoro 69 pamoja na Mablanketi 69. Tunawaomba wadau wa maendeleo kuendelea kutoa msaada kwa watoto hao kwani vifaa vyao vingi vimeungua.”

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Hassan Juma amesema kuwa chuo hicho Kiislamu kina jumla ya wanafunzi 69 na wote wapo salama na tayari wamehamishiwa kwenye jengo jingine kwani hata paa za bweni lao zimeungua hivyo linatakiwa kukarabatiwa upya.

Zifuatazi ji baadhi ya picha za matukio tofauti baada ya ya Moto huo.

Wakandarasi wabanwa Manyara
'Msanii haondoki WCB bure, nimewekeza hela yangu'- Diamond