Bweni la shule ya sekondari ya Kiislam ya African iliyopo maeneo ya Kaloleni mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2020, na kwamba hii ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua.

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, Inspekta Jeremiah Mkomagi, amesema kuwa walipata taarifa za moto huo majira ya saa 1:40 usiku na mpaka wanafika eneo la tukio moto ulikuwa umeshika sehemu kubwa ya bweni.

“Tulipata taarifa kwamba kuna moto katika shule ya sekondari ya African Muslim na tulipofika tukakuta moto ni mkubwa sana na ni jengo la bweni la ghorofa moja na moto ulikuwa umeanzia kwenye moja ya chumba ambacho kinatumika kama stoo”, amesema Inspekta Mkomagi.

“Kwenye tukio hilo hakuna majeruhi wala kifo kwa sababu wanafunzi waliondolewa mapema na kupelekwa sehemu salama, vitu vilivyoungua ni nguo zao, vitanda na madaftari, chanzo hakijabainika kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa shule kuungua na hii ni mara ya tatu” amesema Inspekta Mkomagi.

Uhalifu hauwezi kukufanya ukawa kiongozi - IGP Sirro
WFP waibuka kidedea tuzo ya amani nobel 2020