Zaidi ya Wasichana milioni 4 wamekeketwa nchini Kenya hasa katika Kaunti zilizoko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, ambapo Wadau wanapendekeza kuandaliwa kwa mkakati maalum wa utoaji wa elimu.

Inaarifiwa kuwa, jamii za Mandera na Wajir bado zina idadi kubwa ya visa vya ukeketaji na imebainika kuwamila potofu, kudorora kwa usalama na ukosefu wa fedha, vimelemaza juhudi za kukomesha suala la ukeketezaji huku mamlaka zikipewa wito wa kushugulikia suala hilo.

Ukeketaji ni mila ambayo inapingwa vikali, lakini bado inaendelea kufuatwa na baadhi ya makabila huku Watoto wa kike wakiwa ndio waathirika namba moja wanapofanyiwa vitendo hivyo na baadhi yao hupoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanawake pia bado wanaishikilia mila hiyo na kutaka iendelee kutokana na wao wenyewe kukeketwa wengi wao wakiolewa wakiwa na umri mdogo jambo ambalo limekuwa ni kisababishi mojawapo na kufanya jambo hilo kificho kwa watoto wao.

Job, Lomalisa watamba kuichakaza Al Ahly
El-nino: Wawili wapoteza maisha, Gari lasombwa