Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amewataka Wasichana na Wanawake nchini kuchangamkia fursa zilizopo ili kujikwamua kiuchumi.

Katambi ameyasema hayo wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Wanawake ni jeshi kubwa na Serikali ina matarajio makubwa na kundi hilo katika kuweza kushiriki vema kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi yetu na jamii kwa ujumla.”

Aidha, ameeleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa rasilimali watu ni nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Wachezaji Simba SC wafunguliwa milango
Diarra Djigui awaita mashabiki kwa Mkapa