Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo, Mobhare Matinyi amesema hadi kufikia sasa miili iliyopatikana ni 87 na yote imeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa mazishi.
Matinyi amesema kuwa Kwa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali inagharamia mazishi yote na kutoa mkono wa pole wa shilingi milioni moja (Sh. 1,000,000/-) kwa kila mwili.
Aidha, amesema hadi sasa jumla ya majeruhi na wagonjwa waliopokelewa tangu maafa yalipotokea ni 139 na waliopo Hospitalini ni watu 30 na idadi ya waathiirika walio kambini ni 517.