Watanzania wametakiwa kutokubali kutoa rushwa mahali popote huku akisisitiza kuwa wananchi ni wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya vita hiyo.

Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Nyerere Square, jijini Dodoma.

Amesema, “ninyi ni wadau wakubwa wa kukomesha rushwa. Nyie ni wadau wakubwa wa kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ili nchi yetu isiwe na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi mnapaswa kufichua vitendo vya ukosefu wa maadili na uvunjifu wa haki za binadamu.”

Aidha, Majaliwa ameongeza kuwa, “Mtanzania usikubali kutoa rushwa popote, hasa kwenye maeneo unayopaswa kupewa huduma hiyo. Wewe ni Mtanzania unalindwa na sheria za nchi za kupata huduma bure kama vile hospitali bila kutoa rushwa. Inatakiwa kila Mtanzania abebe jukumu hili kwa mikono miwili, alisimamie na alitekeleze.”

Mvua zinazoendelea: Wananchi watahadharishwa
Athari Mafuriko Hanang': Serikali yawagusa waathiriwa