Bondia wa ngumi za kulipwa Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ amefichua kuwa anahitaji kupata muda wa kutosha kujitafakari kabla ya kuamua kurejea ulingoni kufuatia kupoteza pambano lake la mwisho dhidi ya Erick Tshimanga Katompa, mwezi uliopita mkoani Arusha.

Dullah Mbabe ametoa kauli hiyo kufuatia kupoteza kwa mara ya pili mbele ya Bondia huyo kutoka DR Congo, ambaye kabla ya pambano hilo, Mbabe alikiri wazi kuwa ni ndiyo nafasi yake ya mwisho itakayoweza kurejesha heshima yake lakini mipango ikamgomea.

Dullah amesema kuwa kwa sasa hana lolote la kuweza kusema kwa kuwa mambo yake yalishavurugika hivyo amejipa muda wa kujitafakari kabla ya kuamua hatma yake.

“Siwezi kusema au kufanya jambo lolote kwa sasa kwa sababu hakuna ambaye anaweza kunielewa, ndiyo maana sina ambacho ninachoweza kufanya walimwengu wakanielewa, kiukweli ni jambo gumu.

“Nadhani nahitaji nipate muda wa kutosha kuweza kujitafakari juu ya suala la lini na wakati gani natakiwa kurejea ulingoni ila naweza kusema kwamba nikiwa tayari nitaweka wazi, kauli ya kuwa Penati ya mwisho ni kweli na nilishasema hivyo sina cha kusema.” Amesema Dullah

Young Africans kuitumia Mtibwa Sugar kimataifa
Arteta aendelea kulia na waamuzi, VAR