Kocha Mkuu wa Aresenal Mikel Arteta alitoa majibu yenye utata alipoulizwa mtazamo wake kuhusiana na matukio mawili yaliyoinyima Penati na bao la dakika za mwisho na kusema yalikuwa matukio ya wazi dhidi ya Aston Villa Jumamosi (Desemba 09).

Mwamuzi Jared Gillett na tekilonojia ya marejeo ya matukio kupitia video (VAR) wote waliamua kutoipa Penati Arsenal dakika ya 47 wakati Gabriel Jesus alipoangushwa na Douglas Luiz.

Kisha, walikataa kuipa Arsenal bao la dakika za mwisho lililofungwa, Kai Havertz kwa kigezo mpira ulimgusa mkononi Mshambuliaji huyo kabla ya kufunga.

Akizungumza Arteta alisema: “Ningependa nisizungumze chochote ingawa naona tukio la Penati Iilikuwa la wazi kuliko la mkono la Havertz.

Aliposukumwa zaidi kuongea kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo Arteta alijibu: “Lilikuwa tukio la wazi. Hicho ndicho ninachomaanisha.”

Arteta tayari yuko kwenye mzozo na Chama cha Soka cha England kutokana na matamshi yake ya kukosoa maamuzi ya kuipa Newcastle bao lililofungwa na Anthony Gordon mwezi uliopita.

Kocha huyo pia alikuwa akitumikia adhabu ya kuzuiwa kukaa kwenye benchi la ufundi la Arsenal kwenye mchezo dhidi ya Villa baada ya kupata kadi ya tatu ya njano kwa msimu huu kwenye mchezo dhidi ya Luton katikati ya wiki iliyopita.

Dullah Mbabe aomba muda kujitafakari
ECOWAS yautambua utawala wa Kijeshi Niger