Jumuia ya Uchumi wa Afrika ya Magharibi – ECOWAS, imeutambua rasmi Utawala wa kijeshi wa Niger ingawa imetaka kipindi hicho cha mpito kiwe kifupi kuelekea kwenye utawala wa kiraia ikiwa na lengo la kuilegeza vikwazo vya kiuchumi nchi hiyo.

Maamuzi hayo, yametolea katika mkutano wa kilele wa jumuia hiyo uliofanyika mjini Abuja, Nigeria huku utawala wa kijeshi wa Niger ukisema kuwa unahitaji angalau miaka mitata kuirejesha nchi hiyo kwenye utawala wa kiraia.

Baadhi ya viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wakihudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo mjini Abuja, Nigeria,

Rais wa Kamisheni ya ECOWAS, Omar Touray aliwaambia waandishi wa habari kwamba viongozi wa mataifa ya Benin, Togo na Sierra Leone, wamekabidhiwa jukumu la kuendeleza mazungumzo na baraza la Kijeshi la Niger yatakayoamuwa juu ya uondolewaji wa vikwazo.

Utawala wa kijeshi wa Niger umekuwa ukisema kwamba unahitaji angalau miaka mitatu kuirejesha nchi kwenye utawala wa kiraia. 

Arteta aendelea kulia na waamuzi, VAR
Young Africans yaanza kuiwinda Mtibwa Sugar