Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, Kipchumba Murkomen ameiomba idara ya Polisi kuchunguza uwezekano wa hujuma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kufuatia giza la usiku usiku wa Jumapili ya Desemba 10, 2023 lililosababishwa na kukatika kwa umeme.

Murkomen, ametoa ujumbe huo hii leo Desemba 11, 2023 kutokana na hapo jana hitilafu ya umeme kusababisha nchi nzima kuwa giza kwa takribani saa tatu, ambapo Shirika la Umeme Nchini Kenya – KPLC lilitangaza kuwa hali hiyo ilisababishwa na hitilafu ya mitambo.

Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, Kipchumba Murkomen.

Taarifa, hiyo ya KPLC pia ilibainisha kukatika kwa umeme kwenye eneo lote la Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyattta – JKIA, jijini Nairobi, huku Watu wengi wakihoji tukio hilo la kushangaza wakidai majenereta ya akiba ambayo huwa tayari kwa usaidizi ni kwanini hayakufanya kazi.

Hata hivyo, Wahandisi wa Shilika hilo la Umeme walisema wafafanyia kazi suala hilo na baada ya saa tatu hali ya kawaida ilirejea kwa Umeme kuwaka maeneo yote, hivyo watu kuendelea na shughuli zao za kawaida za kila siku.

Mradi wa Maji Ziwa Victoria kuvinufaisha Vijiji 33
Mvua zinazoendelea: Wananchi watahadharishwa