Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake dhidi ya Wydad A.C, Jumamosi (Desemba 09), ugenini nchini Morocco ambapo timu hiyo ilifungwa bao 1-0.

Matokeo hayo kwenye mchezo wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yanaifanya Simba SC kushika mkia wakiwa na Point mbili huku Asec Mimosas waliopata ushindi wa 2-0 dhidi ya Jwaneng wakiongoza kundi hilo la B kwa kuwa na pointi saba.

Kocha huyo kutoka nchini Algeria amesema baada ya mchezo huo alikaa na wachezaji wake na kuwapongeza kwa kuonyesha kiwango kizuri hasa katika eneo la ulinzi na kiungo na kutengeneza nafasi walizoshindwa kuzitumia.

Benchikha ameongeza kuwa matokeo ya mchezo huo yamempa mwanga kuelekea mchezo wa marudiano Uwanja wa Benjamini Mkapa Desemba 19 na kuahidi kupata ushindi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga Robo Fainali ya Michuano hiyo.

“Tulicheza vizuri, tulizuia na kushambulia kwa kasi, eneo la kuweka mpira nyavuni ndilo tumeshindwa lakini nimeridhishwa na timu ilivyocheza. Mchezo huu umeisha tumerudi nyumbani kujiandaa na mechi ya marudio ambayo tutajipanga vizuri na kuhakikisha nasi tunashinda,” amesema Benchikha.

“Yote yaliyotokea yatatupa usahihi wa maandalizi mazuri ya mchezo ujao. Eneo tulilokuwa bora tutakwenda kuongeza ili kuimarika zaidi na kwenye mapungutu tutakwenda kurekebisha,” amesema Benchikha

Bao liiloizamisha Simba SC kwenye mchezo huo lilifungwa na Zakaria Draoul dakika za nyongeza ambapo alipiga mpira uliopita katikati ya miguu ya kipa Ayoub Lakred.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini mechi ikichezwa zaidi katikati ya uwanja na mlinda mlango, Ayoub Lakred alicheza Penati iliyopigwa na nahodha, Yahya Jabrane dakika ya 41 baada ya Kibu Denis kumchezea madhambi Saifdine Bouhra ndari ya eneo la 18.

Young Africans yaanza kuiwinda Mtibwa Sugar
Matatizo ya Figo: Watu 600 wameomba msaada - Prof. Jay