Mwanamuziki wa Hip hop na aliyekuwa Mbunge wa wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule Maarufu kama Prof. Jay, ameeleza kuwa amepokea maombi mengi kutoka kwa watu tofauti wenye matatizo ya figo muda mfupi baada ya kutangaza kufungua Foundation iliyozinduliwa Dec 10, 2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wazo la kufungua Foundation ni kwa lengo la kusaidia waatu wanaosumbuliwa na matatizo ya figo na ni baaad ya yeye kusumbuliwa na tatizo hilo kwa miaka miwili na kutumia gharama kubwa kupata matibabu.

“Tulifikiria kuanza kuchangisha Tsh. milioni 800, target kuanza na wagonjwa 50, mpaka sasa tumepata maombi kupitia ukurasa wetu wa Instagram kuna watu zaidi ya 600 wanaomba msada na kwaba wana hali mbaya wantegemea Pfor Jay Foundation iwe mwokozi wao,” Amesema Prof. Jay

“Yalisemwa mengi wakati naumwa, nilitobolewa koo na moyo wangu ulisimama mara tatu mungu amesikia kilio na mombi ya watanzania, nimecheki vocal cord na inaonesha kabisa haijaguswa sauti inaendelea kuimarika na itarudi kama zamani”

AidhaRof. Jay amesema kuwa anatoa EP kama zawadi na pia shukrani yake kwa mungu ambapo EP hiyo itaitwa Nusu Peponi Nusu Kuzimu ina nyimbo nne.

Benchikha: Niliwapongeza wachezaji wangu
Simulizi: Akili ndogo inavyoweza kuipiku akili kubwa