Abel Paul, Jeshi la Polisi – Longido.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Longido, limeendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia makundi mbalimbali ya jamii za kifugaji huku wakitumia siku 16 za kupinga vitendo hivyo kuchangia damu katika kituo cha Afya Longido.

Akiongea mara baada ya zoezi hilo Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Leah Ncheyeki amesema Wilaya hiyo kiasili ni jamii ya kifugaji ambayo imekuwa ikiendelea kuziishi tamaduni ambazo baadhi zimekuwa zikiwanyima fursa hususani watoto wakike wa jamii za kifugaji.

Amesema Jeshi la Polisi wilaya hiyo kupitia siku kumi na sita za kupinga ukatili waliona vyema waendelee kutoa elimu kwa jamii hizo za kifugaji ili kuachana na tamaduni ambazo hazina tija kipindi hiki cha mabadiliko ya dunia.

Aidha amebainisha kuwa wataendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii hizo za kifugaji ili waondokane na vitendo hivyo vinavyowanyima fursa ya kufanya maamuzi.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Tarafa Longido, Enna Mtera amesema jamii hiyo imekuwa ikiendekeza mila ambazo zinamnyima haki mwanamke na watoto kwa kufanya maamuzi huku akiwaomba Jeshi hilo waendele kutoa elimu zaidi ili kuikomboa jamii hiyo na mila Potofu.

Rungu la FIFA laiangukia Tabora United
Serhou Guirassy agauka lulu Ujerumani, England