Jeshi la Polisi Nchini Kenya, linamshikilia Afisa wa Polisi wa Kituo cha Nakuru Kostebo Nicholas Masau kwa tuhuma za kusababisha kifo cha muhudumu wa baa kwa kumfyatulia risasi na kuwajeruhi wengine watatu kufuatia mzozo ulioibuka baada ya kukataa kulipa bili ya vinywaji vya Ksh.16,000.

Tukio hilo, liliotokea usiku kuamkia Desemba 13, 2023 ambapo Masau aliliripotiwa kujihususha na mzozo wa Wafanyabiashara wa baa katika klabu ya Vegas ambapo inasemekana alifyatua risasi kabla ya kukimbia.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa,”alizua ugomvi na wahudumu wa baa kwenye baa iliyotajwa kuhusu bili ya vinywaji alivyokuwa amekunywa katika harakati hizo hali ya taharuki ilitokea na afisa huyo akamjeruhi vibaya muhudumu wa baa ambaye ni Anna Maina”

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru alisema Afisa huyo alikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kaptebwa bastola na risasi mbili na magada sita yaliyotumika zilipatikana.

Polisi limesema waliojeruhiwa ni wanawake wawili na Wanaume wawili na marehemu alikuwa Mwananmke na mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo ukisubiri uchunguzi.

Reece James asaka suluhu ya tatizo
Makamba athibitisha kifo cha Mtanzania Israel