Nahodha wa Chelsea, Reece James, anatazamiwa kuonana na mtaalamu wa misuli ya paja katika jitihada za kufahamu tatizo lake la hivi karibuni, lakini kuna uwezekano mkubwa akawa nje ya dimba hadi Februari, 2024.

James ana historia ya matatizo ya misuli ya paja na alitolewa Uwanjani wakati wa kipindi cha kwanza katika mechi ya Ligi Kuu ya England ambayo Chelsea walichapwa na Everton iliyochezwa Jumamosi iliyopita.

Tayari msimu huu, hajacheza kwa miezi miwili kutokana na tatizo sawa na hilo wakati wa mechi ya ufunguzi mwezi Agosti, mwaka huu.

Inaripotiwa James anatarajiwa kukosa kucheza soka kwa takribani miezi mitatu na hataweza kurejea hadi mwisho wa Februari au mwanzoni mwa Machi, 2024.

James mwenye umri wa miaka 24 anakutana na mtaalamu wa misuli ambapo itajumuisha uchunguzi ili kuelewa undani wa tatizo.

Akiwa pia na matatizo mbalimbali ya kifundo cha mguu na goti katika miaka ya hivi karibuni, James anakadiriwa kukosa mechi 35, karibu na msimu mmoja kamili wa Ligi Kuu, kutokana na majeraha ya nyama ya paja pekee.

Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino, alichukizwa na kushindwa kwa hivi punde zaidi kutokana na athari ya kumpoteza mchezaji huyo muhimu na mwenye ushawishi wakati ambapo The Blues wako katika mradi mkubwa wa kujenga timu.

“Bila shaka kwetu sisi ni mchezaji muhimu, mmoja wa mabeki bora zaidi duniani,” alisema Pochettindo.

“Tumesikitishwa kwa sababu unapoamini naweza kujenga kitu na mchezaji kama yeye ambaye anafaa kuwa muhimu kwetu hawezi kuisaidia timu.”

Kwa bahati mbaya kwa Chelsea, mlinzi wa pili wa kulia Malo Gusto anaendelea kukosekana pia.

Mfumo haulengi kumuondoa mtu kazini - Kikwete
Bia yasababisha mauaji, watatu wajeruhiwa