Haruna Juma – Mpanda.

Mbunge wa wa Jimbo la Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi ametoa zaidi ya shilingi milioni 47 zikiwa ni fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya, Maji, Elimu na Barabara Jimboni hapo.

Akikamilisha ziara yake ya siku mbili jimboni humo, Kapufi ametembelea Hospitali ya Manispaa ya Mpanda na kutoa kiasi cha shilingi milioni 6 kwa ajili ya ununuzi wa baadhi ya vifaa katika jengo la upasuaji la Hospitali hiyo.

Aidha ametoa pia kiasi cha shilingi milioni 10, kwa shule mpya ya msingi Kawajense, pkwa ajili ya kuweka uzio na kusema inatakiwa kuwa shule ya mfano, ili kupunguza changamoto ya kutokuharibu miundombinu yake iliyondoa msongamano wa Wanafunzi darasani kutoka 300 kwa darasa moja hadi Wanafunzi 150.

Miradi mingine iliyotembelewa na kupata mgao wa fedha za mfuko wa jimbo hilo ni ujenzi wa Zahanati ya Makanyagio, Choo cha soko la Shanwe, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA shule ya Msingi Kigamboni na utengenezaji wa Madawati ya Shule ya Msingi Msakila na Mkapa

Aidha, Miradi mingine ni ununuzi wa Samani za ofisi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Lyamba na mradi wa ujenzi wa Bweni na vyumba vya Madarasa katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum Azimio.

Miradi mingine ni ujenzi wa choo cha Walimu kituo cha Shule Shikizi Tulieni, ujenzi wa ofisi za Serikali ya Mtaa na Zahanati katika kata ya Uwanja wa Ndege, Kituo cha Afya Nsemulwa, ujenzi wa nyumba ya Walimu yenye uwezo wa kuchukua familia mbili katika shule ya Sekondari Kawalioa na mradi wa Shule mpya ya msingi Kawalioa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madiwani wa kata za Makanyagio, Shanwe, Kawajense, Nsemulwa, Uwanja wa Ndege na Majengo, wamempongeza mbunge huyo kwa namna ambavyo anahakikisha kero za Wananchi zinatatatuliwa kwa wakati.

Mabadiliko: Uhamisho, teuzi za Rais Samia
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 14, 2023