Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini DRC, Corneille Nangaa anayeishi uhamishoni nchini Kenya ametangaza kuundwa kwa muungano wa kisiasa na kijeshi na waasi wa M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha.

Hatua hiyo, imepeleke Sñerikali ya Kongo kuionya Kenya kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kwa kumruhusu Nangaa, ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kongo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018, kuisgi Nchini humo.

Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini DRC, Corneille Nangaa Yobeluo (Picha ya Luis TATO / AFP).

Katika matamshi yake, Kiongozi huyo wa upinzani alitoa wito wa muungano wa vikosi vyote vya kijeshi, kisiasa na kijamii ili kuijenga upya Serikali na kurejesha amani katika taifa hilo lililokumbwa na mapigano ya mara kwa mara hasa maeneo ya mashariki.

Nangaa alisema vikundi tisa vikijumuisha M23, tayari vimeungana naye kupitia muungano wake wa Congo River Alliance akisema unalenga kuleta moja na utulivu wa kitaifa ili kuondoa udhaifu wa Serikali ya Kongo katika muda wa miongo mitatu na kushindwa kwake kudumisha usalama nchini kote.

Ya Kibwetere: Akili za kuambiwa changanya na zako
Watendaji wazembe kazini washikwa pabaya