Afara Suleiman, Hanang’ – Manyara.

Maofisa Maendeleo ya Jamii Nchini – CODEPATA wamekabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mahindi, unga lishe na maziwa kwa ajili ya Watoto vyenye thamani ya shilingi milioni 2.2 kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia waathiirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya tope, Mawe na Maji, Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Kaimu Rais wa chama hicho, Wanchoke Chinchibera amesema wameguswa na tukio hilo na kuamua kijichangisha kuja kuwashika mkono waathiirika hao wa mafuriko, yaliyotokea Desemba 3, 2023 Manyara.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilayani Hanang’, Janeth Mayanja amekishukuru chama hicho kwa namna walivyoguswa na changamoto za Wananchi na kuahidi kuwa misaada hiyo itawafikia walengwa.

Kwasasa Serikali inaendelea kukarabati miundombinu ya barabara katika mji huo wa Katesh, huku wataalamu wengine wakiendelea na tathmini ili kazi ya ujenzi wa makazi mapya kwa ambao Nyumba zao zimeharibika kabisa, ianze mapema Januari 2024.

TFS wakabidhi Madawati Shule mbili za Sekondari Misenyi
MAKALA: Rais Samia anapozibadili fikra hasi kuwa chanya