Mshambuliaji nyota wa Mtibwa Sugar aliyepo kwa sasa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Seif Rashid Karihe, amesemna likizo waliyonayo wachezaji kwa sasa baada ya Ligi Kuu Bara kusimama sio ya kula bata bali kutafakari na kujipanga upya warudi uwanjani wakiwa moto zaidi na walivyofanya hapo awali.

Ligi imesimama kwa muda wa miezi miwili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 na Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2023 zinazoanza rasmi Januari mwakani na inatarajiwakurejea tena Februari na Mtibwa Sugar itavaana na Coastal Union, Februari 23.

Mtibwa haijawa na mwendelezo mzuri, licha ya kumtema aliyekuwa kocha mkuu, Habib Kondo na kumrudisha kikosini, Zubeiry Katwila bado ipo mkiani ikikusanya pointi nane baada ya mechi l4 na kuishi kwa presha ya kuepuka kushuka daraja.

“Hatukai kizembe, tutatumia mapumziko kuumiza kichwa ili kujipanga upya kusudi ligi ikirejea tuwe imara zaidi hata kisaikolojia, hakuna tatizo lolote linatukabili ni matokeo tu ya mpira,” amesema Karihe, aliyefuta wazo la timu hiyo ya Mtibwa kushuka daraja, akisema wataipigania hadi inusurike kama msimu uliopita.

 

Salim Aiyee kurudi Ligi Kuu
Ahmed Ally: Chama ataondoka Simba SC kwa heshima