Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ amesema atarekebisha makosa madogo yalitokea katika pambano lililopita dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Uganda  Mohamed Sebyala.

Twaha Kiduku ambaye alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa PST kupitia pambano hilo lililopigwa katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, amesema alishindwa kumpiga mpinzani wake KO, kutokana na ugumu, ubora na uzoefu aliokuwa nao bondia huyo.

“Nawaomba Watanzania waendelee kunisapoti kwani nimeona kuna mapungufu madogo madogo ambayo nitayafanyia kazi kuhakikisha ninatoa burudani kwa mashabiki wangu,” amesema Kiduku.

Bondia amesema huyo moja ya mipango na mikakati yake ya mwakani kufanya vizuri katika mapambano yake na kuonyesha ubora wa pekee kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki zake.

“Ofa zinakuja nyingi kwangu, lakini uongozi wangu unaangalia pambano lenye maslahi kwangu, siyo nipigane bila mpangilio kwa sababu hii ni kazi kwangu yangu, ninatarajia kufanya mambo makubwa zaidi na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wangu katika mapambano ya mwakani,” amesema.

Dawa za kulevya, ulevi kupindukia chanzo matukio ya uhalifu
MAISHA: Mgahawa unaolipia kinacholetwa si ulichoagiza