Mshambuliaji wa Azam FC Mkongomani, Idris Mbombo inadaiwa ameomba kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliosalia na kikosi hicho kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara chini ya Kocha Mkuu, Youssouph Dabo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema mchezaji huyo amewasiliana na viongozi kwa ajili ya kusitisha mkataba wake ila maamuzi ya mwisho hayajafikiwa japo kuna uwezekano nyota huyo akaachwa.

“Ni kweli mazungumzo hayo yapo na uwezekano wa Mbombo kuondoka dirisha hili ni mkubwa kwa sababu sio mchezaji tegemneo tena kikosini, hivyo tunaweza tukamruhusu ili akatafute changamoto sehemu nyingine” kimeeleza chanzo kutoka Azam FC

Afisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo. Hasheem Ibwe amesema: “Bado tuna mkataba naye wa miezi sita na yeye anafurahia maisha ya hapa, hivyo hizo ni stori tu kama stori nyingine, imani yetu ni kubwa kwake na hatuna wasiwasi juu ya uwezo alionao.” amesema.

Mbombo alijiunga na Azam FC Julai 31, 2021 akitokea El Gounah ya Misri na akihusishwa kutua Nkana ya Zambia aliyoichezea huku Azam FC ikiwa mbioni kukamilisha usajili wa Mshambuliaji Mkolombia, Franklin Navarro kutoka timu ya Cortulua ya Colombia.

Kapera: Nimekuja Geita Gold kufanya kazi
Mexime: Nipeni kwanza muda