Johansen Buberwa – Kagera.

Kilo 1000 za Mchele Mbuzi 20 pamoja na juisi katoni 68 vimetolewa na Rasi Samia Suluhu Hassan kwa vituo vya kulelea watoto yatima 10 Mkoani Kagera vikiwa na thamani ya shilingi 6,800,000 ili kusherekea sikukuu ya Mwaka Mpya 2024.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitu hivyo Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajath Fatma Mwasa amesema Rais Samia amependezw kusherehekea sikukuu na watoto hao.

Katika hatua Nyingine, RC Mwasa ametumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wa Mkoa Kagera heri ya kuelekea kuanza mwaka mpya 2024 akisema anamini utakuwa mwaka wa mafanikio zaidi kuliko mwaka unaoisha.

Kwa upande wao baadhi ya Watoto na Walezi wa vituo hiyo, Daud Amos na Cathelne Gizeri wamemshukuru Rais na uongozi wa Mkoa kwa namna walivyo kumbukwa ili waweze kusherehekea na kufurahia sikukuu kama watu wengine.

Chama, Phiri waipasua Simba SC
Mikel Arteta: Ni aibu kubwa