Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Tanzania Bara, Abdulurhman Kinana amesema ipo haja ya kutoa fursa zaidi kwa Wananchi kujiamulia mambo yanayohusu maendeleo yao.

Kinana ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM na wanachi wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi baada ya kuzindua Shina la CCM Majengo Sokoni.

Amesema, huenda haifanyiki sawa kutowapa wananchi fursa kubwa ya kuamua mambo yanayohusu maendeleo yao, jambo ambalo linasababisha kutofikia ufumbuzi wa baadhi ya changamoto katika vitongoni, vijiji au mitaa.

Kinana yupo Wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikakazi ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa ambao pia utahudhuriwa na Mbunge wa Ruangwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 

Wawili kuongeza nguvu Dodoma Jiji FC
Makala: Afrika inavyoisubiri shida ili ipate maarifa