Jumuiya ya Kampuni za Uwindaji wa Kitalii Nchini -TAHOA, imetoa pole ya Shilingi 47,409,800 kwa Wanahanang’ waliopatwa na maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope na mawe Mkoani Manyara na kusababisha vifo, majeruhi, uharibifu wa miundombinu na mali.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa TAHOA, Abdulkadir Mohamed amesema pole hiyo inaambatana na michango iliyotolewa na makampuni ya uwindaji kwa namna walivyoguswa, ili kununua vifaa vya ujenzi wa nyumba za waathirika.

“Sisi kwa umoja wetu tumechanga fedha za ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambavyo vitapelekwa Hanang hivyo tumeungana na Serikali kwa kuamua kukabidhi mchango wetu utakaosaidia wananchi wa Katesh Hanang kurejesha hali zao za maisha katika ubora zaidi,” amesema Abdulkadir.

Akitoa neno la Shukrani mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama aliishukuru kampuni ya TAHOA kwa namna walivyojitoa kuungana na Serikali kurejesha hali ya awali hasa makazi ya watu wa Hanang.

Mexime: Ihefu itafanya vizuri Ligi Kuu
Coastal Union kurudi kambini, wawili wasajiliwa