Ukosoaji umeendelea dhidi ya Rais wa Kenya, William Ruto kutokana na kauli aliyoitoa kuwa Serikali yake haitaheshimu maamuzi ya Mahakama, yatakayopinga miradi, huku akiwashatumu baadhi ya Majaji kwa wafisadi na kutojali maslahi ya umma.

Hatua hiyo inakuja baada ya Jumanne wiki hii Januari 2, 2024 Ruto kudai baadhi ya majaji wanashirikiana na wanasiasa wa upinzani pamoja na watu wengine kwa nia ya kuzuia uendelea wa miradi ya Serikali.

Hata hivyo, akijibu shutuma hizo za Rais Ruto Jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome wakati alisema kukiuka maauzi ya Mahakama ni kinyume cha sheria.

Aidha, Koome pia aliwataka Majaji wa Mahakama kuendelea na kazi yao kwa mujibu wa sheria za nchi bila ya uoga wala upendeleo, huku Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga akisema uamuzi wa Ruto ni hatari kwa demokrasia.

 

Fumua fumua yanukia Mtibwa
Mexime: Ihefu itafanya vizuri Ligi Kuu