Rais wa Kenya, William Ruto  amemtaka mtangulizi wake  Uhuru Kenyatta kuacha kushirikiana na kinara wa upinzani na Kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ili kutekeleza maandamano ambayo yamesababisha vifo na uharibifu wa mali.

Ruto, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mji wa Mai Mahiu uliopo kaunti ya Nakuru Mkoa wa bonde la ufa, na kudai kuwa Uhuru amekuwa akifadhili kwa siri maandamano ya Odinga dhidi ya serikali, ambayo amesema  yamekuwa yakileta madhara.

Mstaafu Uhuru Kenyatta (kushoto), akiwa na Rais William Ruto.

“Nataka nimwambie rafiki yangu Uhuru, ata wewe wachana na huyu mzee (Odinga), wacha kumpatia pesa ya kununua watu wa Mungiki wachome Nairobi. Wewe umekuwa rais, kuwa mungwana, tulikuunga mkono ulikuwa rais wetu, uliunga mtu wa kitendawili mkono tukamwangusha, wachana na yeye,”  alisema.

Aidha, Ruto ameongeza kuwa ingawa kufanya maandamano ni haki ya raia yeyote kikatiba, lakini Odinga atakabiliwa vikali na vyombo vya usalama iwapo umwagaji damu zaidi utashuhudiwa katika maandamano mengine yaliyopangwa kufanyika tena siku chache zijazo.

Miradi ya maji: Aweso awashukia Wahandisi
Watanzania msikubali kupotoshwa - Chongolo