Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto – UNICEF, limesema watoto 289 wanaaminika kufariki katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023 wakati wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya.

Taarifa ya UNICEF imeeleza kuwa, idadi hiyo ya vifo ni mara mbili zaidi ya ile  iliyorekodiwa katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2022.

Kufuatia hatua hiyo, UNICEF imehimiza kuwekwa kwa njia salama na za kisheria kwa watoto wanaojaribu kuingia Ulaya kwa ajili ya kutafuta usalama wa maisha yao.

Hata hivyo, Afisa wa UNICEF anayehusika na masuala ya uhamiaji, Verena Knaus amesema idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi kwani kuna baadhi ya ajali za boti kwenye bahari ya Mediterania ambazo hazinakiliwi.

Watanzania msikubali kupotoshwa - Chongolo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 16, 2023