Afrika ina makabila mengi yaliyotawanyika katika maeneo mbalimbali yaliyosheheni mila, desturi na tamaduni tofauti, ambapo mengine huwa na sifa au muonekano wa kipekee wa kimaumbile, nikimaanisha unaweza kuwagundua kwa muonekano wao au rangi yao, urefu wao, ufupi wao lugha nk.

Makala haya hii leo, yatakuongoza kwenye kulifahamu kabila la Dinka ambalo lenyewe hujulikana kwa kuwa na Watu warefu zaidi barani Afrika wakitokea nchi ya Sudan ya Kusini wakiaminika kuwa ndio watu warefu zaidi barani Afrika na urefu wao ni wa kustaajabisha.

Wadinka sio tu watu warefu zaidi barani Afrika, lakini pia wao ni kama sehemu ya kabila la Nilotic, wanaunda kabila kubwa zaidi nchini Sudan Kusini. asili yao ni uchungaji wa jadi na ukulima ukiwa ndio utambulisho wao thabiti wa kitamaduni.

Urefu.

Wana urefu wa wastani wa futi 6, au mita 1.83, kwa wanaume na futi 5, inchi 10, au mita 1.78, kwa wanawake na utambulisho wao mwingine ni ngoma zao za kitamaduni na muziki ambao huwa sehemu muhimu ya utamaduni wao, naweza sema Wadinka hawa wana historia kubwa zaidi.

Hata hivyo, uchunguzi wa kianthropometriki uliochapishwa mwaka wa 1995 unaonesha kuwa kimo cha sasa cha wanaume wa Dinka ni cha chini ikihisiwa kuwa inatokana na utapiamlo au migogoro inayoendelea nchini humo, na ulionesha kuwa wana urefu wa wastani wa sentimita 176.4 (5 ft 9.4 in).

Lakini hii haibadilishi hadhi yao kama watu warefu zaidi barani Afrika, kwani tafiti zingine zimeonyesha kuwa data linganishi za urefu wa kihistoria na lishe huwaweka Wadinka kama watu warefu zaidi duniani ingawa pia hili halijathibitishwa rasmi.

Tmaduni.

Jambo moja linaloonekana kuwahusu Wadinka ni kwamba wao hawana mamlaka ya kisiasa na badala yake, jamii yao inaundwa na koo nyingi zinazojitegemea lakini zilizounganishwa zikijihusisha sana na mambo ya Kilimo na Ufugaji kwa sehemu kubwa.

Baadhi ya koo zao, huwa na machifu wa kitamaduni, wanaojulikana kama “Mabwana Wakubwa wa Mkuki wa Uvuvi” au beny bith, ambao hutoa uongozi kwa watu wote na wanaonekana kuwa warithi kwa sehemu.

Historia ya Watu wa Dinka.

Hadithi na simulizi zinasema kwamba Wadinka walitokea eneo Gezira nchini Sudan katika Ufalme wa Alodia, aliyekuwa Mkristo akimiliki himaya ya makabila mbalimbali iliyotawaliwa na Wanubi na alitawala eneo hili wakati wa enzi za kati.

Kupitia mwingiliano wao na Wanubi, na kwa kuwa kwenye mpaka wao wa kusini, watu wa Dinka walipata sehemu kubwa ya leksimu ya Kinubi na baada ya Alodia kusambaratika katika karne ya 13, Wadinka walianza kuondoka Gezira, wakiepuka uvamizi wa watumwa, migogoro ya kijeshi, na ukame.

Ingawa inaamini katika MUNGU mmoja tu muumbaji, Nhialic anasimama kwenye kichwa cha Miungu ya Dinka, wakiamini kwamba Nhialic mara nyingi hukaa mbali na watu na huepuka kuwasiliana nao moja kwa moja.

Moja ya kanuni kuu za dini ya Dinka ni dhabihu ya ng’ombe, ambapo “Mabwana Wakubwa wa Mkuki wa Uvuvi” kwa kawaida hufanya dhabihu na suala la umri huwa jukumu kubwa katika mtindo wa maisha wa Dinka.

Kuhusu imani.

Kwa Vijana wanaoingia utu uzima wanapitia mila ya jando ambayo inahusisha kuweka alama kwa kifaa chenye ncha kali kwenye paji la uso. Pia hupokea jina la pili la rangi ya ng’ombe kwenye hafla hii wakiamini kwamba badala ya kuwa na kitabu cha dini, asili na mazingira yao huwapa nguvu ya kiroho.

Ama hakika Afrika ina makabila mengi yaliyotawanyika katika maeneo mbalimbali yaliyosheheni mila, desturi na tamaduni tofauti, ambapo mengine huwa na sifa au muonekano wa kipekee wa kimaumbile, nikimaanisha unaweza kuwagundua kwa muonekano wao au rangi yao, urefu wao, ufupi wao lugha nk.

Malumbano hayawezi kupewa nafasi - Rais Dkt. Samia
Sakata la Bandari: Serikali ifanyie kazi maoni ya Wananchi - Lusinde