Kama tulivyoona katika sehemu ya kwanza la makala hi kuwa Bara la Afrika linajulikana ulimwenguni kwa sifa nyingi ikiwemo utajiri wa rasilimali, umaskini, ukosefu wa usalama na ufisadi.

Tuliona kwamba hili limefanya baadhi ya maeno kuwa maarufu kulingana na sifa mojawapo kati ya hizo chache zilizo orodheshwa na sehemu hiyo ya kwanza tulimuangalia muasisi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Hayati Nelson Mandela maarufu kama Madiba.

Mandela alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, lakini kabla ya kuwa rais alipigana dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na kujitolea sehemu ya maisha yake ya utu uzima kukaa gerezani kwa miaka 27.

Hata hivyo, itambulike kuwa Viongozi wa awali wa nchi nyingi za Bara la Afrika wengi walikuwa ni wanaharakati na si wanasiasa ambapo mara nyingi wanaharakati whuwa na tabia za kuangalia maslahi ya umma na si yao binafsi.

Leo tuone machache kumuhusu Mkongwe Haile Selassie, yeye alikuwa ni mtawala wa Ethiopia kuanzia mwaka 1916 hadi 1974 na baadaye kuwa mfalme (1930-1974).

Selassie alikuwa ni mwanachama wa mwisho wa nasaba ya Solomoni ya taifa hilo lililopo ukanda wa Afrika ya Mashariki na wakati wa utawala wake, Ethiopia ilishuhudia mageuzi makubwa ya kielimu kwani shule nyingi zilikuwa zikijengwa.

Hata hivyo, ukosefu wa haki wa kijamii ulianguka na vikosi vya usalama vya serikali viliimarishwa ili kuondoa kasoro hiyo na kusababisha hali kuwa shwari kwa mara nyingine.

Haile Selassie pia alikuwa katika mrengo wa Pan-Africanist ambaye alisukuma kusudio la kuundwa kwa Umoja wa Afrika, akijenga mtandao mpana wa uhusiano na jumuiya za Kiafrika katika ughaibuni pamoja na visiwa vingine vya Karibea.

Hadi leo, jumuiya ya Rastafari mara nyingi inamchukulia kama masihi aliyezaliwa upya.

Itaendelea………..

Serikali yaridhishwa maendeleo ujenzi kituo cha afya
Nani kusonga Fainali UCL leo City, Madrid, Inter na Milan