Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Senga Gugu amesema ameridhishwa na hatua ya Ujenzi wa kituo cha Afya Chipanga na ununuzi wa vifaa tiba katika Zahanati hizo chini ya ufadhili wa KOIKA na UNICEF.

Gugu ameyasema hayo Mei 15, 2023 wakati wa ziara yake ya  ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya ikiwa ni sehemu ya ziara za kikazi katika Mkoa wa Dodoma.

“kila sababu ya sisi kujiridhisha kwamba hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi zimefikia wapi ili tuone tunaendaje mbele katika kukabidhiana, kama tulivyosema kuna baadhi ya maeneo yanatakiwa kuimarishwa zaidi kabla ya huduma hazijaanza kutolewa kwenye maeneo hayo “amefafanua Gugu.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu akikagua Ujenzi wa kituo cha Afya Chipanga kilichopo Wilaya ya Bahi, tarehe 15 Mei 2023. Kituo cha Afya hicho tayari kimesha kamilika na baadhi ya Majengo Huduma zimeshaanza kufanyika na ujenzi wake umefadhiliwa na KOIKA na UNICEF.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha zilizofanikisha uboreshaji wa miundombinu ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ikiwemo manunuzi ya vifaa tiba na Shirika la UNICEF kwa kufadhili mradi huo ambao utaboresha huduma za dharura za afya ya uzazi na mtoto katika Kata ya Chipanga na Kata za jirani.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongella na Bi. Siwema Jumaa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba na watumishi wengine wakikagua kituo cha Afya Soya kilichopo Wilaya ya Chemba, Mei 15, 2023.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala Gugu ametembelea pia vituo vilivyoengwa katika Wilaya Chamwino na Chemba ambavyo ujenzi wake umekamilika na unategemewa kunufaisha wakazi wa Wilaya za Jirani.

Utekelezaji wa Miradi hiyo katika Wilaya zote tatu umefanyika sambamba na ununuzi wa Vifaa Tiba na Jenereta la Kutumia wakati wa dharura na Mafunzo ya Huduma za dharura kwa watumishi, Mradi huo Ulioanza Kutekelezwa  Julai 2021 na Utatakiwa kukamilika kabla ya Juni 10, 2023.

TAMWA-ZNZ yawataka Wanawake kutotumiwa
Viongozi 10 waliozibeba nchi zao Barani Afrika – 2