Ikiwa imesalia miaka miwili ili Watanzania watekeleza haki yao ya kikatiba kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025, Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt, Mzuri Issa amewataka wanawake wenye nia za kugombea kutokubali kutumiwa na wenye ajenda zao, zikiwemo za kukwamisha wanawake kutoshika nafasi za uongozi.

Dkt. Issa ameyasema hayo wakati alipokua akizungumza na wanawake kutoka vyama mbali mbali vya siasa Zanzibar katika ofisi za chama hicho Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa akizungumza na baadhi ya wanawake watia nia kutoka vyama mbali mbali vya siasa Zanzibar katika ukumbi wa Chama hicho Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Amesema, licha ya kuwa Zanzibar ina idadi kubwa ya wanawake wengi zaidi lakini kwa mshangao mkubwa bado wanawake hao hawapati nafasi ya kuchaguliwa kutokana na kasoro mbali mbali zikiwemo za mitazamo hasi iliokua ikitawala kwenye jamii.

Aidha ameongeza kuwa, ili wanawake welio wengi waweze kufanikiwa kwenye uchaguzi huo hawana budi wao wenyewe kushikana na kuwa wamoja zaidi na kukataa kabisa kubaguliwa.

Mwakilishi mstaafu jimbo la Magomeni chama cha Mapinduzi CCM Hafsa Said Khamis akitoa ushuhuda katika harakati zake za uongozi.

Awali akitoa ushuhuda wa mafanikio, aliyewahi kuwa mgombea wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi kwa nafasi ya uwakilishi jimbo la Magomeni mwaka 1995, Hafsa Said Khamis amesema wanawake hawakuweza kupaza sauti, kwenye mazingira ambayo yeye alithubutu.

Serikali yatoa ufafanuzi kufungia baa, kumbi za starehe
Serikali yaridhishwa maendeleo ujenzi kituo cha afya