Serikali nchini, imeshauriwa kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na Watanzania wenye nia njema kuhusu sakata la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salam na kuyafanyia kazi na iachane na mambo mengine ikiwemo kutoa elimu.

Ushauri huo umetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa, Livingstone Lusinde katika mkutano wa Baraza kuu la Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM Wilaya ya Bariadi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa, Livingstone Lusinde.

Amesema, “maoni yametolewa mengi ya viongozi wa dini, ya wanasheria, ya wasomi, serikali iyachukue na kuendelea kufanya kazi ilizojipangia, hivi kama kwenye mpira wa mguu kusingekuwa na refa wa kuamua magoli mpira ungechezwaje?.”

Aidha, Lusinde ameongeza kuwa Serikali imeshayasikia maoni hayo hivyo yachujwe na yenye nia njema yafanyiwe kazi na kufunga ajenda hiyo ili kuendelee na kazi nyingine, huku Mbunge wa Viti maalum Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss akiwataka Watanzania kutokubali Muungano wa Tanzania utikiswe.

Makala: Fahamu kabila la watu warefu zaidi barani Afrika
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 15, 2023