Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar mpya itakuwa na usafiri wa umma wa mabasi ya umeme, treni pamoja na Taxi za baharini na kwamba Serikali itasaini mradi wa kituo cha usafiri wa baharini eneo la Mpiga Duri Januari 9, 2024.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Soko kuu la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B , Mkoa wa Mjini Magharibi katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema, ametimiza ahadi aliyoitoa kwa wafanyabiashara wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi Mwaka 2020 ikiwemo kuwajengea mazingira bora ya kufanyia biashara, kuwawezesha kwa mitaji na vitendea kazi.

“Serikali imetimiza ahadi yake kwa kutoa mikopo inayofikia bilioni 25 kuwawezesha wajasiriamali nchini na halikadhalika wavuvi, wakulima wa mwani wamepatiwa boti bila kuwasahau waendesha bodaboda,” alisema.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia ametoa kipaumbele kwa Wafanyabiashara wa awali wa soko la Mwanakwerekwe baada ya kukamilika Mwezi Machi kati ya wafanyabiashara 5,000 watakaoingia kwenye soko hilo.

Vyuo vikuu wahimizwa matumizi sahihi Vifaa vya Mawasiliano
Mahundi ampa siku saba Meneja wa RUWASA Lushoto