Timu za Morocco na Guinea Bissau zimekuwa za kwanza kuwasili nchini Ivory Coast tayari kwa fainali za 34 za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazoanza Jumamosi (Januari 13).

Kwa mujibu wa ratiba ya kuwasili kwa timu shiriki iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’, mabingwa watetezi wa AFCON 2021, Senegal watawasili katika ardhi ya Ivory Coast kesho Jumanne (Januari 09) wakati Morocco iliyocheza nusu fainali ya Kombe la Dunia ilitua jana Jumapili (Januari 07) tayari kwa mchezo wao wa ufunguzi Januari 13, 2023.

Timu hiyo iliyocheza Robo Fanali katika michuano iliyopita nchini Cameroon, iko katika Kundi F pamoja na mabingwa mara mbili Congo DR, washindi wa mwaka 2012 Zambia na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Guinea Bissau itacheza dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo Januari 13, 2024 kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara huko Ebimpe.

Mabingwa mara tatu Nigeria na Guinea ya Ikweta, wenyewe wanakamilisha idadi ya timu za Kundi A.

Simba SC kuisaka Nusu Fainali Zanzibar
Kikosi kazi Taifa Stars AFCON 2023