Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Adel Amrouche ameweka hadharani kikosi cha wachezaji 27 watakaowakilisha Tanzania kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ä°vory Coast zitakazoanza Jumamosi (Januari 13).

Katika kikosi hicho, Amrouche amewaacha Abdul Seleman Sopu’, Metacha Mnata, Khelfin Hamdoon na Twariq Abdillahi.

Awali kocha huyo alitangaza majina 55 baadae yakapunguzwa kabla ya kuondoka kwenda kuweka kambi Misri na kubaki 31 kujiandaa na fainali hizo, zitakazoanza Januari 13 hadi Februari 11 mwaka huu.

Katika kurasa za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ wamechapisha orodha ya mwisho ya wachezaji 27 watakaovaa jezi ya Tanzania kwenye mashindano ya AFCON 2023.

Makipa: Kwesi Kawawa, Beno Kakolanya na Aishi Manula,

Mabeki: Haji Mnoga, Ibrahim Hamad, Dickson Job, Novatus Dismas, Abdi Banda, Lusajo Mwaikenda, Miano Danilo, Abdulmalik Zakaria, Mohamed Hussein na Bakari Mwamnyeto.

Viungo: Mudathir Yahya, Feisal Salum, Himid Mao,Tarryn Allarakhia, Mzamiru Yassin, Morice Abraham, Sospeter Bajana na Mohamed Sagaf.

Washambuliaji: Kibu Denis, Cyprian Kachwele, Mbwana Samatta, Simon Msuva, Charles M’mombwa na Ben Starkie.

Kanuni zinataka majina kati ya 24 na 27 lakini ni 23 tu watakaoruhusiwa kucheza mashindano.

Taifa Stars ambayo inashiriki mashindano hayo ya 34 mchezo wa kwanza watacheza Januari 17 dhidi ya Morocco, mchezo wa pili Januari 21 dhidi ya Zambia na mchezo wa tatu Januari 24 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC).

Hii ni mara ya tatu Tanzania inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ ambayo itafanyika katika miji sita ya Abidjan, Yamoussoukro, Bouaké, San-Pédro, Korhogo na San-Pédro.

Morocco, Guinea Bissau zatangulia AFCON 2023
Wanafunzi waongezewa likizo