Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wamepanga kusubiri hadi diirsha lijalo la majira ya kiangazi, ili kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani, Joshua Kimmich, ambapo wanaamini watampata kwa pesa kiduchu zaidi.

Kimmich ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2025, mwisho wa msimu huu huenda akauzwa kwa pesa kiduchu zaidi ya ilivyo sasa.

Man City walihitaji kumsajili Kimmich kwenye dirisha hili lakini inaonekana kuwa ngumu kwa mabosi wa Munich kukubali kumuachia kutokana na umuhimu wake kwenye timu.

Taarifa za awali zilidai kwamba Man City huenda ikawasilisha ofa ya zaidi ya Pauni 44 milioni kwa ajili ya kumnasa staa huyu mwenye umri wa miaka 28, lakini inaaminika msimu ujao huenda bei hiyo ikapungua zaidi.

Matumaini ya kuipata saini yake yanaonekana kuwa makubwa zaidi kwa sababu ya uhusiano kati ya timu hizo mbili zilizofundishwa na Pep Guardiola.

Mfaume Mfaume amuibua Pialali bifu la Mwakinyo
Okrah aibuka mapyaa Young Africans