Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali amevunja ukimya kwa kuingilia kati ugomvi wa Hassan Mwakinyo na Twaha Kiduku kwa kumwambia Mfaume Mfaume atulize mdomo wake kwa kuwa hata yeye alishawahi kumbadili jina wakati wa pambano lao.

Pialali ametoa kauli hiyo kufuatia Mfaume Mfaume kuingilia ugomvi wa Mwakinyo na Kiduku ambao umeambatana na maneno yanayoonekana kuwa makali upande wa Twaha Kiduku hali iliyopelekea Pialali kuvunja ukimya huo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Pialali amefichua kuwa anashangaa kuona Mfaume ameingilia ugomvi ambao siyo wake huku akisahau hata yeye aliwahi kumuita dada pili badala ya jina lake halisi lakini alichukulia ni sehemu za tambo katika kuamsha mchezo huo.

“Nashangaa kuona Mfaume Mfaume amekuwa kimbelembele kumsema vibaya Mwakinyo ikiwa aliyeambiwa anapaka piko ni Twaha Kiduku kiasi cha kutaka kuona dunia inamchukia jambo ambalo siyo sawa kwa upande wake.

Sioni kama sawa anachofanya Mfaume, mwaka Juzi yeye mimi aliniita dada Pili badala ya Pialali lakini hakuna ambaye alimwambia amekosea, anachotakiwa kujua ni kwamba maneno ya Mwakinyo kwa Kiduku ni sehemu ya kuhamasisha mchezo wa ngumi,” amesema Pialali.

Mwakinyo awakataa mabondia wachambuzi
Mpango mkakati umesitishwa