Bondia Hassan Mwakinyo ametoa ombi kwa Promota wa pambano lake la January 27, 2024 kati yake na Bondia Miya NKanku kutoka Congo kwamba hataki Wachambuzi wa pambano hilo wawe Mabondia wenzake kutoka Tanzania wanaotumika kwenye mapambano mengine.

Pambano hilo litapigwa New Amaan Complex Zanzibar na tayari Shirikisho la Ngumi Duniani (WBO) limeridhia liwe la kuwania ubingwa wa WBO Africa likiwa ni pambano la round 10 uzito wa kilo 72.

Mwakinyo amenukuliwa akisema “Ombi la wazi kwa Promota Semunyu kutoka Familia ya Mogadishu pamoja na Mimi C.E.O wao, hatutaki Wachambuzi Mabondia mnaowatumia kwenye mapambano mengine,”

“Ikiwa itawaridhia Azam TV wakupe Kamati yao ya Wachambuzi yani Patrick Nyembela na Team yake ni Watu wamekuwa na utashi wa juu zaidi na ikiwa hakuna budi awepo Bondia basi kura zangu Naseeb Ramadhani, namba moja na ukikosa kabisa majibu, nitakuletea wachambuzi wa ngumi kutoka Tanga”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 9, 2024
Mfaume Mfaume amuibua Pialali bifu la Mwakinyo