Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange ametangaza msako wa kuwakamata Wazazi wote wenye Wanafunzi wanaotakiwa kuanza shule kwa madarasa ya awali msingi na Sekondari, ambao bado hawataripoti hadi ifikapo januari 15 2024.

Twange ameyasema hayo baada ya kukagua baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati, ikiwemo Shule ya msingi Queen Sendiga na Shule ya Sekondari kololi zilizopo Kata ya Maisaka Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Amesema, mahudhurio ya Wanafunzi yanaridhisha kwa shule zote za Msingi na Sekondari lakini hiyo haifanyi wale wasiowapeleka shule watoto wakaacha jambo hilo na hivyo wahakikishe wanatekeleza agizo hilo kwa wakati.

Twange pia amesisitiza kuwa mara baada ya muda huo kupita, msako wa kuwakamata utaanza nyumba kwa nyumba katika Mitaa na Vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Mahakama yafikiria kumuachia Mhubiri tata Mackenzie
Polisi wahofia idadi ya vifo wanaojinyonga kila wiki