Wazazi na Walezi wa Wanafunzi aa Shule Za Msingi na Sekondari Wilayani Babati Mkoani Manyara wameiomba Serikali kuboresha Miundombinu ya Barabara na Maji, ili Watoto wao waweze kuwa na ustawi mzuri kitaaluma.

Wakizungumza katika kikao mara baada ya Wanafunzi kurejea Shuleni kuanza Muhula mpya wa Masomo wa 2024, wamesema miundombinu ya Barabara na ukosefu wa Maji ni kikwazo kwa Wanafunzi nyakati za Mvua.

Kufuatia malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange alielezea mikakati ya Serikali juu ya utatuzi wa kero hizo na kusema zitafanyiwa kazi kwa wakati.

Aidha, katika hatua nyingine Twange ametoa onyo kwa Wazazi au Walezi wasiopeleka Watoto Shule na kusema Serikali itaanza msako wa kuwakamata.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 10, 2024
Wanafunzi waambiwa ukatili sasa basi