Takriban Wahamiaji wasiopunguwa 6,618 walikufa au kutoweka wakijaribu kuingia Uhispania kupitia njia ya bahari mwaka 2023.

Shirika la kutetea haki za Wahamiaji Nchini Hipania, limesema idadi hiyo ni mara tatu zaidi ya iliyorekodiwa mwaka 2022, ambapo wahamiaji 2,390 walipoteza maisha.

Aidha, katika idadi hiyo, Watoto 384 ni miongoni mwa wahanga, taarifa iliyotokana na mahojiano kutoka kwa familia za waathiriwa pamoja na takwimu zinazotolewa na maafisa wa shughuli za uokoaji.

Hata hivyo, vifo vingi vya idadi ya wahamiaji iliyotajwa, vimetokea katika Bahari ya Atlantiki, ambayo inatumiwa kama njia ya kutoka Afrika kuingia visiwa vya Canary Nchini Hispania.

Ataka Wazazi wawalinde Watoto umri wa balehe
Mahakama yafikiria kumuachia Mhubiri tata Mackenzie